Kituo cha Utamaduni cha China nchini Tanzania chaandaa maonyesho ya sanaa ili kuimarisha uhusiano wa kitamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2022
Kituo cha Utamaduni cha China nchini Tanzania chaandaa maonyesho ya sanaa ili kuimarisha uhusiano wa kitamaduni
Watembeleaji wa maonyesho wakitazama michoro ya Tingatinga kwenye Kituo cha Utamaduni cha China nchini Tanzania kilichoko katika Mji wa Dar es Salaam, Tanzania, Novemba 1, 2022. Kituo cha Utamaduni cha China nchini Tanzania kimeandaa maonyesho ya kazi za sanaa yaliyopewa jina la “Tanzania yenye Haiba - Maonesho ya Michoro ya Tingatinga na Maonyesho ya Vinyago vya Ebony” kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kitamaduni kati ya nchi hizo mbili. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

DAR ES SALAAM - Kituo cha Utamaduni cha China nchini Tanzania kimeandaa maonyesho ya kazi za sanaa yaliyopewa jina la “Tanzania yenye Haiba - Maonyesho ya Michoro ya Tingatinga na Maonyesho ya Vinyago vya Ebony” kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kitamaduni kati ya nchi hizo mbili.

Maonyesho hayo yaliyofunguliwa Jumanne mjini Dar es Salaam, ambao ni mji mkubwa zaidi wa Tanzania, yameonyesha kazi muhimu za sanaa kutoka Tanzania na China, kuthamini jukumu la sanaa na utamaduni katika maelewano na urafiki wa kimataifa.

Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Sanaa la Taifa la Tanzania (BASATA), Auleria Dotto, amesema kazi za sanaa ya Tingatinga zimekuwa na soko kubwa nchini China tangu mwanzoni mwa Mwaka 2000. Michoro ya Tingatinga na uchongaji wa vinyago ni aina za Sanaa za kipekee na zenye mvuto wa kimataifa nchini Tanzania.

Dotto amekishukuru Kituo cha Utamaduni cha China, na Ubalozi wa China nchini Tanzania hasa, kwa kukuza na kuendeleza kazi za sanaa za Tingatinga.

Joseph Kahama, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kuhimiza Urafiki kati ya Tanzania na China, amesema sanaa na picha za kuchora zinakwenda kwa urefu na kina katika kuelewa utamaduni.

Konsela wa Utamaduni wa Ubalozi wa China na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Tanzania, Wang Siping amesema kituo hicho kimemwalika msanii wa Tingatinga kuonesha kazi 30 za sanaa, huku Zhang Jingnan raia wa China ambaye amekaa Tanzania kwa miaka mingi pia amealikwa kuonyesha mkusanyo wake wa vinyago vya ebony.

Wang amesema wawili hao wameanzisha maonyesho ya kudumu ya nakshi ya vinyago vya ebony huko Beijing na Changchun nchini China, baada ya kutoa mchango mkubwa katika kupanua ushawishi wa aina hii ya sanaa nchini China na hata duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha