China kuondoa ushuru kwa asilimia 98 ya bidhaa za Uganda zinazouzwa China

(CRI Online) Novemba 25, 2022

Ubalozi wa China nchini Uganda na wizara ya biashara, viwanda na ushirikiano ya Uganda, zilifanya hafla huko Kampala ya kutangaza sera ya kuondoa ushuru kwa asilimia 98 ya bidhaa za Uganda zinazouzwa nchini China. Balozi wa China nchini Uganda Bw. Zhang Lizhong alipohutubia hafla hiyo, alisema hatua hiyo ya kuondoa ushuru kwa aslimiza 98 ya bidhaa za Uganda zinazouzwa nchini China ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye ufunguzi wa mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la ushirikuano kati ya China na Afrika (FOCAC), ambako alisema kupanua sera ya kuondoa ushuru wa bidhaa zinazouzwa nchini China kwa nchi zilizoko nyuma kiuchumi. Mwaka huu inatimia miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Uganda. China ni soko kubwa lenye watu zaidi ya bilioni 1.4, China inataka Uganda itumie vizuri sera husika kuwanufaisha watu wa nchi mbili kupitia bidhaa zenye ubora zinazouzwa nchini China, na kuchangia zaidi kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Waziri wa biashara, viwanda na ushirikiano wa Uganda Bw. Francis Mwebesa amesema Uganda inathamini uhusiano mzuri uliopo kati yake na China, na kuisifu China kwa msaada wake wa muda mrefu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Uganda. Ametoa wito kwa wadau wa makampuni ya Uganda watumie vizuri sera hiyo, kuzidi kuuza bidhaa zenye ubora kwa China, kuhimiza biashara na uwekezaji kati ya nchi mbili, na kuhamasisha maendeleo na ushirikiano kati ya pande mbili kwenye sekta za fedha, sayansi na teknolojia, na utalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha