Misri yafukua jengo la mazishi ya watu wa Kale wa Greco-Roman

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2022
Misri yafukua jengo la mazishi ya watu wa Kale wa Greco-Roman
Picha hii isiyo na tarehe ikionyesha eneo la kiakiolojia la jengo kubwa la mazishi ya watu wa kale wa Greco-Roman huko Fayoum, Misri. Misri imetangaza Desemba 1 kugunduliwa kwa mabaki ya jengo kubwa la mazishi ya watu wa kale wa Greco-Roman katika Mkoa wa Fayoum, kusini mwa mji mkuu Cairo. (Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Misri/Kutumwa Xinhua)

CAIRO - Misri imeitangaza Alhamisi kugunduliwa kwa mabaki ya jengo kubwa la mazishi ya watu wa kale wa Greco-Roman katika Mkoa wa Fayoum, Kusini mwa Mji Mkuu Cairo.

Ugunduzi huo umefanywa katika misheni ya kiakiolojia ya Misri kwenye eneo la Makaburi ya Garza huko Fayoum iliyoanza Mwaka 2016, imesema taarifa ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Misri.

"Picha kadhaa, sanamu ya Isis-Aphrodite, mchanganyiko wa mungu wa kike wa Misri ya kale Isis na Aphrodite wa Kigiriki, jeneza la mbao, jeneza lenye umbo la mwanadamu na rekodi zilizotengenezwa na mafunjo ambazo zinarejelea hali ya kijamii, kiuchumi na kidini ya wakaaji wa kipindi hicho, vimepatikana ndani ya jengo hilo," taarifa hiyo ya wizara imesema.

Sakafu ya jengo hilo imetengenezwa kwa vigae vya rangi na vilivyopambwa vya chokaa vinavyoelekea kwenye barabara nyembamba, na mabaki ya nguzo nne kupatikana ndani ya nyumba ya mazishi, imeongeza taarifa.

Kijiji cha Garza, kilichojulikana kwa jina la Philadelphia katika enzi ya Himaya ya Ugiriki ya kale, kilianzishwa katika Karne ya Tatu KK kikiwa ni eneo kuu la mradi wa ukarabati wa jangwa na Ptolemy II Philadelphus, ambaye pia alijulikana kama Ptolemy the Great, kwa ajili ya kupata rasilimali za chakula, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha