Baraza la Usalama la UM lakaa kimya kwa dakika moja kuomboleza kifo cha Jiang Zemin

(CRI Online) Desemba 02, 2022

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano lilikaa kimya kwa dakika moja ili kuomboleza kifo cha aliyekuwa rais wa China Jiang Zemin.

Mwenyekiti wa zamu wa Baraza hilo ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Ghana katika Umoja wa Mataifa Balozi Harold Adlai Agyeman, amesema Jiang Zemin alitoa mchango mkubwa katika kuhimiza mageuzi na ufunguaji mlango, ujenzi wa mambo ya kisasa na maendeleo ya uchumi nchini China, na vilevile amani, usalama na maendeleo ya dunia. Jumuiya ya kimataifa itamkumbuka Jiang Zemin kwa mchango wake, na kifo chake ni hasara kubwa kwa China na kwa jumuiya ya kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha