Vyombo vya habari vya Kenya: Afrika yanufaika na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”

(CRI Online) Desemba 02, 2022

Gazeti la Nation la Kenya limetoa makala likisema pendekezo la China la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limeleta manufaa makubwa kwa nchi za Afrika haswa Kenya.

Makala hiyo yenye kichwa cha Pendekezo la China la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” laleta Manufaa kwa Afrika, inasema kupitia pendekezo hilo, nchi za Afrika zimepata uwekezaji kwa wingi, na miundombinu yao zikiwemo bandari, reli, barabara, mawasiliano ya habari na nishati imeboreshwa.

Makala hiyo inasema Kenya ni moja ya nchi zilizonufaika zaidi na pendekezo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha