Tanzania itaweka bango la Kiswahili juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2022

Tanzania itaweka bango la Kiswahili juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro, ambacho ni mlima wa juu kabisa barani Afrika, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha siku ya uhuru, Desemba 9 ya nchi hiyo.

Jumamosi iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, James Mdoe akikabidhi bango hilo kwa timu ya wapanda milima katika Dodoma, Mji Mkuu wa Tanznaia .

“Wizara yetu imepewa heshima ya kufundisha lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi, na tuna sababu ya kutosha ya kuheshimu Lugha ya Kiswahili tunapoadhimisha siku ya uhuru,” alisema Mdoe.

Lugha ya Kiswahili ni moja kati ya lugha zinazotumiwa na watu wengi zaidi barani Afrika, zikijumuisha lahaja muhimu zaidi ya kumi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha