Panda wakubwa waunganisha China na Ubelgiji kwa ushirikiano wa bioanuwai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2022
Panda wakubwa waunganisha China na Ubelgiji kwa ushirikiano wa bioanuwai
Panda mkubwa "Bao Mei" akila mlo wa siku ya kuzaliwa katika bustani ya wanyama ya Pairi Daiza huko Brugelette, Ubelgiji, Agosti 6, 2022. (Xinhua/Zheng Huansong)

BRUSSELS - Panda ni ishara yenye nguvu linapokuja suala la uhifadhi wa spishi. Nchini Ubelgiji, bustani ya wanyama ambayo ni mwenyeji wa panda watano wakubwa na imefanya kazi na wataalam wa wanyama wa China juu ya ufugaji wa panda kwa miaka mingi inaonyesha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kulinda wanyama na kuhifadhi bioanuwai.

Famila ya panda watano

Mwezi Februari mwaka huu, bustani ya wanyama ya Pairi Daiza iliyoko Manispaa ya Brugelette Kusini-Magharibi mwa Ubelgiji ilisaini makubaliano na Shirikisho la Uhifadhi wa Wanyamapori la China kumruhusu Panda Tian Bao mwenye umri wa miaka 6, ambaye ni panda mkubwa wa kwanza kabisa kuzaliwa katika nchi hiyo ya Ulaya, kuendelea kubaki huko, na kuifanya bustani hiyo ya wanyama kuwa mojawapo ya bustani chache duniani zinazokaribisha panda wengi kama watano hivi.

Siku za nyuma Mwaka 1987, panda walianza kupata mashabiki nchini Ubelgiji wakati nchi hiyo ilipopokea panda wawili kutoka Mkoa wa Sichuan Kusini-Magharibi mwa China kwa matembezi ya miezi kadhaa. Wenyeji wengi walimiminika kwenye bustani ambapo walikaa ili kutazama.

Kwa sasa panda hao wamekuwa maarufu sana.

"Kila siku ni tofauti na kamwe huchoki kuchunga wanyama hawa wa ajabu. Na furaha hii inaongezeka mara kumi tunapoweza kuwepo wakati wa kuzaliwa kwa panda," anasema Robin, mlinzi wa panda aliyeonyeshwa kwenye tovuti rasmi ya bustani hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake kamili.

Familia ya panda inayoendelea kukua inaonyesha urafiki kati ya Wachina na watu wa Ubelgiji, na kuweka mfano mpya wa ushirikiano kati ya nchi mbili juu ya uhifadhi wa viumbe hai.

Ushirikiano wa Bioanuai

Ingawa ufugaji wa panda wakubwa wakiwa kifungoni ni mgumu sana, Panda Xing Hui na Hao Hao wamefanikiwa kuzaa watoto kutokana na juhudi za pamoja zilizofanywa na wataalamu wa wanyama kutoka China na Ubelgiji, jambo ambalo linachukuliwa kuwa muujiza.

Mwezi Februari 2016, timu ya wataalam wa China walifika Ubelgiji kusaidia ufugaji wa panda, kwa ushirikiano na wenzao kutoka mbuga ya wanyama na Kitivo cha Mifugo cha Ubelgiji cha Chuo Kikuu cha Ghent. Miezi minne baadaye, Panda Tian Bao alizaliwa, ambaye jina lake kwa Lugha ya Kichina linamaanisha hazina kutoka mbinguni.

Zaidi ya hayo, Panda Bao Di na Bao Mei walizaliwa Mwezi Agosti 2019, ambao walitungwa mimba ya kuzaliwa kwao kwa njia ya kueneza kwa msaada wa wataalamu kutoka kituo cha China. Katika hafla ya Tuzo za Dunia za Giant Panda Mwaka 2019, jozi hiyo ya panda wachanga ilishinda Tuzo ya Dhahabu ya "Vitoto vya Panda vya Mwaka". 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha