Naibu Waziri Mkuu wa Laos apongeza Reli ya Laos-China akiita fahari ya Laos

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2022
Naibu Waziri Mkuu wa Laos apongeza Reli ya Laos-China akiita fahari ya Laos
Msichana na mhudumu wa Shirika la Reli la China-Laos wakipiga picha mjini Luang Prabang, Laos, Aprili 24, 2022. (Picha na Yang Yongquan/Xinhua)

VIENTIANE - Naibu Waziri Mkuu wa Laos Sonexay Siphandone Jumamosi alisifu reli ya Laos-China akiita fahari ya Laos.

Alipokuwa akihutubia mkusanyiko wa watu kwa hiari wakati akikagua utendakazi wa reli hiyo Desemba 3, 2021, Sonexay amesema reli hiyo ya kuvuka mpaka, ambayo ni mradi wa kihistoria wa urafiki kati ya Laos na China, ni mradi wa kimkakati wa kubadilisha Laos kutoka kuwa nchi isiyo na bandari hadi kitovu cha mawasiliano kilichounganishwa na sehemu mbalimbali, kinachoshirikiana na Mpango uliopendekezwa na China wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Sonexay, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi cha Laos (LPRP), amesema uendeshaji wa reli hiyo umeimarisha sana nafasi ya kimkakati ya kimataifa ya Laos, na hivyo kuifanya Laos kuwa kitovu muhimu cha usafirishaji katika eneo hilo.

Amesema katika mwaka uliopita, Reli ya China-Laos imekuwa ikiendelea vizuri, ikitoa huduma bora kwa usafirishaji wa abiria na mizigo na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Laos.

Xiang Fangqiang, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Laos, amesema China iko tayari kushirikiana na Laos ili kuhakikisha uendeshaji wa reli hiyo kwa usalama na ufanisi, na kuimarisha uhusiano wa reli ya China-Laos-Thailand, hivyo kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye muunganisho wa kikanda na ustawi.

Ju Guojiang, Mwenyekiti wa Shirika la Reli ya Laos-China (LCRC), ambalo ni shirika la ubia lenye makao yake makuu mjini Vientiane ambalo linahusika na uendeshaji wa sehemu ya reli ya Laos, amesema tangu operesheni yake mwaka mmoja uliopita, reli hiyo imebeba jumla ya abiria milioni 1.269, tani milioni 1.9955 za bidhaa, ikijumuisha zaidi ya tani milioni 1.5761 za bidhaa za kuvuka mpaka.

Ju amesema kuwa kampuni hiyo pia imesaidia kuwaandaa wataalamu na mafundi wa reli wenyeji, na kutoa nafasi za ajira zaidi ya 100,000.

Reli ya China-Laos yenye urefu wa kilomita 1,035 inaunganisha Kunming, Mji Mkuu wa Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, na mji mkuu wa Laos, Vientiane.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha