Mwili wa Jiang Zemin wachomwa Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2022
Mwili wa Jiang Zemin wachomwa Beijing
Xi Jinping, Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, Wang Qishan, Hu Jintao, na wengine wakitoa heshima zao za mwisho kwa Komredi Jiang Zemin katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Desemba 5, 2022. Mwili wa Jiang Zemin, aliyefariki Jumatano iliyopita, umechomwa kwenye Makaburi ya Mapinduzi ya Babaoshan, Magharibi mwa Beijing siku ya Jumatatu. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Mwili wa Rais wa zamani wa China Jiang Zemin, aliyefariki Jumatano iliyopita, umechomwa kwenye Makaburi ya Mapinduzi ya Babaoshan, Magharibi mwa Beijing siku ya Jumatatu.

Jiang alikuwa kiongozi bora aliyefurahia heshima ya juu inayotambuliwa na Chama kizima cha Kikomunisti cha China (CPC), jeshi zima na watu wa China wa makabila yote.

Alisifiwa kama mfuasi mkubwa wa Umarx na mwanamapinduzi, mwanasiasa, mwana mikakati wa kijeshi, na mwanadiplomasia. Jiang alikuwa mpiganaji wa kikomunisti aliyejaribiwa kwa muda mrefu na kiongozi bora wa lengo kuu la ujamaa wenye umaalumu wa China. Alikuwa kiini cha kizazi cha tatu cha uongozi wa pamoja wa Chama na mwanzilishi mkuu wa Nadharia ya Uwakilishi Mtatu.

Xi Jinping, Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, Wang Qishan, na wengine walikwenda katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kutoa heshima zao za mwisho kwa Komredi Jiang kabla ya kuusindikiza mwili wa Jiang kwenye Makaburi ya Mapinduzi ya Babaoshan kwa ajili ya kuchomwa moto.

Hu Jintao pia alikwenda hospitali kutoa heshima zake za mwisho kwa Jiang.

Katika ukumbi kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho, kulikuwa kumening’inizwa bango leusi lenye maandishi meupe yanayosomeka "Utukufu wa milele kwa Komredi Jiang Zemin." Chini ya bango hilo kulikuwa na picha kubwa yenye rangi ya Jiang.

Mwili wa Jiang, ukiwa umefunikwa na bendera ya CPC, ulikuwa katikati ya maua na miberoshi ya kijani kibichi kila wakati.

Askari wa gwaride la heshima walisimama pande zote mbili. Mbele ya jeneza lenye mwili wa Jiang kulikuwa na maua yaliyopangiliwa yaliyowasilishwa na mkewe, Wang Yeping, na wanafamilia wengine, yakiwa na utepe wa hariri wenye maneno "Utaishi mioyoni mwetu milele."

Ndani ya ukumbi huo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kulikuwa na mashada ya maua yaliyotolewa na Xi Jinping, Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, Wang Qishan na Hu Jintao; na Kamati Kuu ya CPC, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC), Baraza la Serikali, Kamati ya Taifa ya Mkutano wa Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC), Kamati Kuu ya Kijeshi, vyama visivyo vya kikomunisti, Shirikisho la Viwanda na Biashara la China, mashirika ya watu, na watu wa makundi mbalimbali katika mji mkuu wa China.

Saa 4 Asubuhi saa za Beijing, Xi Jinping, Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, Wang Qishan, Hu Jintao, na wengineo waliingia ukumbini kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho hospitalini. Walikuwa na maua meupe yaliyobandikwa kifuani mwao na walivaa utepe mweusi mikononi. Walisimama kimya mbele ya mwili wa Jiang.

Xi na wengine waliinama mara tatu kwa Jiang kutoa heshima zao za juu na kutoa heshima kubwa kwake. Baadaye, Xi na wengine walitoa salamu za rambirambi kwa mke wa Jiang na jamaa wengine. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha