Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania atoa rambirambi kwenye Ubalozi wa China kutokana na kufariki dunia kwa Komredi Jiang Zemin

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2022
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania atoa rambirambi kwenye Ubalozi wa China kutokana na kufariki dunia kwa Komredi Jiang Zemin
(Picha inatoka tovuti ya Ubalozi wa China nchini Tanzania.)

Tarehe 5, Desemba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Stergomena Lawrence Tax alikwenda kwenye Ubalozi wa China nchini Tanzania kutoa rambirambi kutokana na kufariki dunia kwa Komredi Jiang Zemin.

Bi. Tax akiweka maua kwa heshima mbele ya picha ya Komredi Jiang, alisimama kimya mbele ya picha yake, na kuandika maneno kwenye kitabu cha rambirambi. Alisema, “ Nikiwa kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, ningetoa salamu za rambirambi kwa huzuni kubwa kwa serikali ya China, Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa China, na kuwapa pole kwa dhati kwa jamaa zake waliofiwa. Hayati rais Jiang Zemin alitoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya Tanzania na China, atakumbukwa daima na watu wa Tanzania.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha