China yasema Ushirikiano wa Marekani na Ulaya haupaswi kulenga upande mwingine wa tatu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2022

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning Jumatatu alisema kuwa ushirikiano kati ya Marekani na Ulaya haupaswi kulenga upande wowote wa tatu.

Msemaji huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari alipotoa maoni yake kuhusu shutuma zilizoibuliwa dhidi ya China zinazotoka katika Mkutano wa Nne wa Ngazi ya juu wa Majadiliano kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya kuhusu China mapema mwezi huu.

"China inakataa kwa uthabiti uingiliaji wa Marekani na Umoja wa Ulaya katika masuala ya ndani ya China na kuichafua China," Mao amesema wakati akijibu.

Wakati Marekani na EU zinasema zitazingatia "kulinda kiini cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa", ni Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya ambazo zimepuuza kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa kama vile utatuzi kwa njia ya amani wa migogoro ya kimataifa na hakuna kuingiliwa kwa mambo ya ndani ya nchi na hata kushambulia kivita nchi huru kama vile Iraq na Syria kwa kisingizio cha haki za binadamu, Msemaji Mao amesema.

"Ikiwa kuna nchi inataka kujadili kushurutishwa kiuchumi, Marekani imelazimisha hadharani nchi kuacha kutumia vifaa vilivyotengenezwa na kampuni za China na kusitisha ushirikiano na China," Mao amesema.

Marekani imeanzisha Sheria ya CHIPS na Sayansi, imeshirikisha washirika wake katika uonevu wa kiuchumi dhidi ya China na kutaka kuitenga na kuikata kwenye minyororo ya ugavi. Sheria ya Marekani ya Kupunguza Mfumuko wa Bei inalazimisha makampuni ya Ulaya kuhamishia mitambo yao ya uzalishaji Marekani. Yote hayo ni mifano ya ushurutishaji wa kiuchumi, amesema.

"Ushirikiano wa Marekani na Umoja wa Ulaya haupaswi kulenga upande wowote wa tatu, bado utafute kutengeneza masuala na China au kuzua makabiliano," amesema Mao.

Zikiwa ni pande zenye nguvu kubwa duniani, Marekani na EU zinahitaji kuonyesha uwajibikaji na kufanya mambo zaidi ambayo yanafaa kwa utulivu na ustawi wa Dunia, ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha