Waziri wa afya wa Tunisia apongeza timu ya madaktari wa China kwa huduma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2022
Waziri wa afya wa Tunisia apongeza timu ya madaktari wa China kwa huduma
Waziri wa Afya wa Tunisia, Ali Mrabet (wa nne, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na madaktari wa China huko Tunis, Tunisia, Desemba 5, 2022. Mrabet alikutana na kundi la 26 la Timu ya Madaktari wa China nchini Tunisia Jumatatu, na kupongeza huduma yake ya kipekee katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini. (Xinhua)

TUNIS - Waziri wa Afya wa Tunisia Ali Mrabet amekutana na Kundi la 26 la Timu ya Madaktari wa China nchini Tunisia siku ya Jumatatu, na kupongeza huduma yake ya kipekee katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Katika hafla ya kuipongeza timu ya madaktari inayomaliza muda wake, Mrabet amesema wajumbe wote wa timu ya China walishikilia nafasi zao kwa kasi wakati wa janga la UVIKO-19 na walitoa mchango mkubwa kwa afya ya Watunisia.

China imetuma wahudumu wa afya zaidi ya 1,100 nchini Tunisia kwa takriban miaka 50, waziri huyo amesema, huku akibainisha utendaji bora wa wahudumu wa afya wa China unajumuisha kiini cha ushirikiano wa tiba kati ya China na Tunisia.

Xu Chuyang, mkuu wa timu ya madaktari wa China, amesema madaktari wa timu hiyo, daima wakishikilia imani kwamba madaktari hawagenganishwa na mipaka na maisha ndiyo ya kwanza, hawajaacha juhudi zozote kumtibu kila mgonjwa.

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, timu ya madaktari wa China imetoa huduma za matibabu kwa zaidi ya watu 100,000 nchini Tunisia, amesema Xu.

Ameongeza kuwa madaktari wa China pia walishiriki na madaktari wa eneo hilo uzoefu wao katika kupambana na janga la UVIKO-19, walitibu wagonjwa wa UVIKO-19, na walitoa masanduku 210 ya vifaa tiba.

Zaidi ya hayo, timu ya madaktari ya China imefanya vikao 12 vya mashauriano ya matibabu bila malipo katika jumuiya za mitaa, shule, na nyumba za ustawi, na kuleta huduma zao kwa watu wengi zaidi nchini Tunisia, Xu ameongeza.

Kundi la 26 la timu ya madaktari wa China liliwasili Tunisia Desemba 2021 na limekuwa likifanya kazi katika miji minne nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha