Reli ya Qingdao-Jinan: Daraja la chuma lenye historia zaidi ya miaka 100 laonekana kwa sura mpya baada ya kukarabatiwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2022
Reli ya Qingdao-Jinan:  Daraja la chuma lenye historia zaidi ya miaka 100 laonekana kwa sura mpya baada ya kukarabatiwa
Tarehe 5, Desemba, wajenzi wa Idara ya 14 ya Kampuni ya Reli ya China wakifanya kazi ya kubadilisha boriti za daraja la boriti za chuma cha pua la Barabara ya Pwani ya Qingdao.

Siku hiyo, kazi ya kubadilisha upya boriti za daraja la boriti za chuma cha pua la Barabara ya Pwani ya Mji wa Qingdao, Mkoa wa Shandong ilikamilika kwa mafanikio. Kwa kufahamishwa, daraja hilo lilijengwa Mwaka 1901, kwa kuwa na historia ndefu na upungufu wa uwezo wa kubeba mzigo, limekuwa na hatari ya usalama. Wajenzi wa reli walihakikisha kazi ya kubomoa boriti za zamani na kuweka boriti mpya kwa mbinu za kiteknolojia ili kulikarabati upya kama lilivyokuwa la zamani, na kuhakikisha treni zinapita salama kwenye reli hiyo katika sehemu hii.

(Mpiga picha: Li Ziheng/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha