UNICEF yahimiza kutoa msaada kwa watoto katika Pembe ya Afrika

(CRI Online) Desemba 06, 2022

Shirika la Kuwahudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetoa ombi la ufadhili wa dharura wa dola bilioni 1 za kimarekani ili kuwasaidia mamilioni ya watoto katika Pembe ya Afrika mwaka kesho.

Shirika hilo limesema, limebadilisha ombi lake la dharura la kuokoa maisha nchini Ethiopia, Kenya na Somalia kwa kutoka dola milioni 879 za kimarekani mwezi wa Septemba hadi dola bilioni 1 za kimarekani kwa ajili ya mwaka mzima wa 2023.

Limesema, watoto wa Pembe ya Afrika wanakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika nchi hizo tatu pamoja na mapigano yanayotokea kaskazini mwa Ethiopia.

Shirika hilo pia limesema, katika mashariki na kusini mwa Afrika litahitaji zaidi ya dola bilioni 1.6 za kimarekani mwaka 2023 kutoa msaada wa uokoaji kwa watu zaidi ya milioni 39.8, wakiwemo watoto zaidi ya milioni 27.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha