Mkutano wa kuomboleza kifo cha Hayati Jiang Zemin wafanyika Beijing

(CRI Online) Desemba 06, 2022

(Picha inatoka CRI.)

Mkutano wa kuomboleza kifo cha rais wa zamani wa China Hayati Jiang Zemin aliyefariki dunia Tarehe 30, Novemba akiwa na umri wa miaka 96, umefanyika leo asubuhi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la China jijini Beijing.

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Rais wa China Xi Jinping ameongoza mkutano huo.

Washiriki wote kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la China walisimama na kukaa kimya kwa dakika tatu kutoa heshima kwa Hayati Jiang kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha