China yaanzisha kazi ya utafiti wa kisayansi kwenye Mlima Qomolangma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 23, 2023

https://english.news.cn/20230522/316a318b75ee455d8475a767c0f1c735/edb95240d981470f9bb2741eddb11d17.jpg

Watafiti wa kisayansi wakijifunza kuweka kituo cha hali ya hewa cha kiotomatiki karibu na kambi ya msingi ya Mlima Qomolangma katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini Magharibi mwa China, Mei 9, 2023. (Xinhua/Jigme Dorje)

https://english.news.cn/20230522/316a318b75ee455d8475a767c0f1c735/95dea7af649241d69ec706e5019e1fae.jpg

Mtafiti wa kisayansi akipima ubora wa maji karibu na kambi ya msingi ya Mlima Qomolangma ulioko Mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China, Mei 14, 2023. (Xinhua/Sun Fei)

https://english.news.cn/20230522/316a318b75ee455d8475a767c0f1c735/acaef4baf1d8411bb03262127e78f529.jpg

Mtafiti wa kisayansi akifanya kazi karibu na kambi ya msingi ya Mlima Qomolangma ulioko Mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China, Mei 15, 2023. (Xinhua/Jigme Dorje)

https://english.news.cn/20230522/316a318b75ee455d8475a767c0f1c735/f88a76354c7d464599cdf7986a45092a.jpg

Watafiti wa kisayansi wakijadiliana kwenye Mlima Qomolangma wenye urefu wa mita 5,300 kutoka usawa wa bahari katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China, Mei 14, 2023. (Xinhua/Sun Fei)

https://english.news.cn/20230522/316a318b75ee455d8475a767c0f1c735/c4932005e00f4bf4b22a208bcfe03126.jpg

Mtafiti wa kisayansi akiendesha droni kwa ajili ya kukusanya sampuli ya hewa katika kituo cha uchunguzi na utafiti wa hali na mazingira cha eneo la Mlima Qomolangma Mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China, Mei 10, 2023. (Xinhua/Jigme Dorje)

KAMBI YA MSINGI YA Mlima QOMOLANGMA, Tibet - Wanasayansi wa China wameanza kazi ya utafiti wa kisayansi katika eneo la Mlima Qomolangma ulioko Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini-Magharibi mwa China ikiwa ni sehemu ya utafiti wa pili wa kina wa kisayansi kwenye Uwanda wa Qinghai-Tibet.

Jumla ya wanasayansi 170 wanafanya utafiti kuhusu maji, ikolojia na shughuli za binadamu, wakilenga kubainisha utaratibu wa mabadiliko ya mazingira na kuboresha mfumo wa ukingo wa usalama wa ikolojia kwenye uwanda huo.

Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet ambao pia unaitwa "paa la Dunia" na "mnara wa maji wa Asia," ni ukingo muhimu wa usalama wa ikolojia nchini China. Pia ni maabara ya asili ya kufanya utafiti juu ya mabadiliko ya Dunia na maisha, mwingiliano kati ya nyanja na uhusiano kati ya mwanadamu na Dunia.

Kwa mujibu wa sheria ya uhifadhi wa ikolojia kwenye Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, China inahimiza na kuunga mkono uchunguzi na utafiti wa kisayansi kwenye eneo hilo la tambarare, na kuhimiza utafiti wa muda mrefu ili kufahamu asili ya ikolojia ya uwanda huo na mabadiliko yake.

Kama sehemu muhimu ya utafiti wa pili wa kina wa kisayansi kwenye Uwanda wa Qinghai-Tibet, ulioanzishwa Mwaka 2017, utafiti huo unaoendelea una umuhimu mkubwa katika kuchunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na mazingira katika eneo la Mlima Qomolangma kwenye maeneo mengine ya Dunia.

Utafiti wa Mlima Qomolangma wa Mwaka 2023 utaendelea kuweka mkazo katika masuala makuu ya kisayansi kama vile jinsi mazingira ya mwinuko wa juu sana ya Mlima Qomolangma yanavyobadilika chini ya ushawishi wa ongezeko la joto duniani, jinsi mabadiliko ya mazingira ya Mlima Qomolangma yanavyoingiliana na pepo za magharibi na monsuni, na jinsi gani mazingira ya Mlima Qomolangma yataathiri mabadiliko ya "mnara wa maji wa Asia," kwa mujibu wa Yao Tandong, mwanataaluma katika Taasisi Kuu ya Sayansi ya China na kiongozi wa timu ya utafiti huo wa pili wa kina wa kisayansi kwenye Uwanda wa Qinghai-Tibet.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha