China kuendelea kuzisaidia nchi zinazoendelea kwa kupeleka timu za msaada wa matibabu

(CRI Online) Mei 31, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema, China itaendelea kuzisaidia nchi zinazoendelea na kuboresha afya na maisha ya watu duniani kupitia timu za msaada wa matibabu za China ambazo kwa sasa wanatekeleza majukumu yao kwenye sehemu 115 katika nchi 56 duniani.

Mao amesema, hivi karibuni, nchi nyingi zimesifu kazi zinazofanywa na timu za matibabu za China katika nchi hizo. Amesema miaka 60 iliyopita, China ilituma timu yake ya kwanza ya matibabu nje ya nchi, na tangu wakati huo, jumla ya wahudumu wa afya 30,000 wa China wametibu zaidi ya wagonjwa milioni 290 katika nchi na sehemu 76, zikiwemo nchi za Afrika na Asia, na kupata mafanikio makubwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha