人民网首页

Teknolojia

Utengenezaji wa barafu kwenye Olimpiki ya Majira ya Baridi ya 2022 wasifiwa kuwa rafiki kwa mazingira

BEIJING – Ikiwa imejizatiti kuandaa Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya majira ya Baridi isiyo na uchafuzi kwa mazingira, Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022, siyo tu imefanya viwanja vya ubora vya barafu vinavyofaa kwa michezo husika katika kumbi za mashindano, lakini pia imezingatia utengenezaji wa barafu ulio rafiki kwa mazingira. Nyuma ya mchakato huo wa utengenezaji barafu kuna aina mbili za friji - kaboni dioksidi - CO2 (R744) na R449A, ambazo zilichaguliwa na kamati ya maandalizi kufuatia mashauriano ya kina na wataalam kutoka ndani na nje ya nchi.

(Picha inatoka IC Photo.)

Roboti kuhudumia wateja kwenye Migahawa ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing

Picha hizo zikionesha mgahawa wa waandishi wa habari wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijng 2022. Kwenye mgahawa huo vifaa vyote vya kujiendesha, na vya akili bandia vinaweza kutoa huduma ya chakula kwa masaa 24, ili kuhakikisha mchakato mzima wa kutoa oda, kupika, na kupeleka chakula unaweza kumalizilika kwa kujiendesha.

Teknolojia za akili bandia yatumiwa katika uendeshaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022

Kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, vifaa hivi vya teknolojia vitawashangaza watazamaji sana! Mfumo wa kutumia carbon dioxide kuzalisha barafu, ambao utoaji wa kaboni karibu sifuri Hii ni ndani ya jumba la kitaifa la michezo ya mbio ya kuteleza kwenye barafu. (People’s Daily Online/Hu Xuerong) Jumba la kitaifa la michezo ya mbio ya kuteleza kwenye barafu linaloitwa “Njia ya Hariri ya Barafu” linazalisha barafu kwa kutumia carbon dioxide, ambayo si kama tu haiharibu tabaka la ozoni bali pia kuwa na ufanisi wa juu zaidi wa kuzalisha barafu.

1