Utengenezaji wa barafu kwenye Olimpiki ya Majira ya Baridi ya 2022 wasifiwa kuwa rafiki kwa mazingira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2022

BEIJING – Ikiwa imejizatiti kuandaa Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya majira ya Baridi isiyo na uchafuzi kwa mazingira, Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022, siyo tu imefanya viwanja vya ubora vya barafu vinavyofaa kwa michezo husika katika kumbi za mashindano, lakini pia imezingatia utengenezaji wa barafu ulio rafiki kwa mazingira.

Nyuma ya mchakato huo wa utengenezaji barafu kuna aina mbili za friji - kaboni dioksidi - CO2 (R744) na R449A, ambazo zilichaguliwa na kamati ya maandalizi kufuatia mashauriano ya kina na wataalam kutoka ndani na nje ya nchi. Kati ya viwanja tisa vya barafu katika kumbi saba za Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022, tano zimetumia CO2 katika kutengeneza barafu, na nyingine nne zimetumia R449A. Ni mara ya kwanza mfumo wa utiaji baridi wa asilia wa CO2 unatumiwa kwenye Michezo ya Olimpiki.

Kwa hakika, ni friji R507 ambazo zilizingatiwa kwanza wakati waandaaji walipoanza kupanga mpango wao wa kutengeneza barafu. R507 inatumika kwa wingi kote duniani na inakidhi matakwa ya Mkataba wa Dunia wa Mazingira wa Montreal kuhusu Vitu Vinavyopunguza Tabaka la Ozoni kwa nchi zinazoendelea.

Ikizingatiwa kuwa R507 ina Uwezo wa Juu wa Kuongeza Joto duniani (GWP) wa 3985, Kamati ya Maandalizi ya Olimpiki ya Beijing 2022 hatimaye iliamua kugeukia teknolojia za kijani ambazo ni rafiki kwa mazingira.

Maeneo ambayo yanahitaji kutengeneza na kudumisha barafu mwaka mzima, ikiwa ni pamoja na Jumba la Taifa la Kuteleza kwa Kasi kwenye barafu, hutumia jokofu asilia CO2. Kinyume chake, kumbi ambazo hutengeneza barafu mara chache, kama vile Kituo cha Taifa cha kuogelea na Jumba la Michezo la Taifa, hutumia friji za kawaida.

CO2 ina Uwezo sifuri wa Kupungua kwa Ozoni (ODP) na GWP wa 1. Ni jokofu nyuma ya mfumo wa majokofu wa CO2, ambao ulipendekezwa kuwa suluhisho la kutengeneza barafu kwa Jumba la Taifa la Kuteleza kwa Kasi kwenye barafu na jopo linalojumuisha wanataaluma kadhaa wa Akademia ya Uhandisi ya China na Akademia ya Sayansi ya China, wataalam waandamizi kutoka ndani ya China wa Shirikisho la majokofu na wawakilishi wa timu ya ujenzi.

Kama ilivyodhihirishwa na Zhang Xinrong, profesa wa Chuo Kikuu cha Peking na mtaalam maarufu wa uhandisi wa joto na majokofu asilia, mfumo wa majokofu wa CO2 unajivunia usalama wa juu, matumizi ya chini ya nishati na gharama ndogo ya uendeshaji na rafiki kwa mazingira. Aidha, joto linalotokana na mchakato huo linaweza kutumika tena, hali ambayo huongeza ufanisi wa usimamizi wa nishati, upozaji na upashaji joto. Mfumo huo ni mojawapo ya teknolojia zenye matumaini zaidi katika usimamizi wa nishati ya maeneo ya barafu na matarajio ya matumizi yake ni makubwa duniani kote.

"Wataalamu kutoka mashirikisho ya kimataifa walituambia kwamba kutumia mbinu za kawaida za kutengeneza barafu ambazo ni rafiki kwa mazingira zitatosha kwa Jumba la Taifa la Kuteleza kwa Kasi kwenye barafu kufikia viwango vya Olimpiki. Lakini tulitumia miezi 18 kusoma nyaraka za kutengeneza barafu kutoka kwa Michezo ya Majira ya baridi ya Olimpiki iliyopita na kuchambua faida na hasara za kila aina ya friji. Hatimaye, tuliweza kupata suluhu bora zaidi," Song Jiafeng, mhandisi wa timu ya ujenzi ya Jumba la Taifa la Kuteleza kwa kasi kwenye barafu anasema.

Kwa mujibu wa Song, kutumia CO2 kama jokofu kunaweza kuongeza ufanisi wa kutengeneza barafu kwa asilimia 30 na kuokoa karibu kilowati milioni mbili za umeme kwa mwaka.

Waandaaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 walikuwa na majadiliano na tafiti za upembuzi yakinifu na kampuni zinazotoa vifaa, wahandisi na watoa huduma wa majumba ya michezo na kuamua kutumia R449A.

R449A ni mbadala wa GWP ya chini kwa R507 duniani kote kama ilivyothibitishwa na mashirika ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Kiyoyozi, Kupasha joto na Jokofu. R449A ina GWP ya 1282, asilimia 68 chini ya ile ya R507.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha