Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la14 la China, akiongoza mkutano wa tatu wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING – Tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la Umma la 14 la China, imefanya mkutano wake wa tatu siku ya Jumapili ambapo Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo, aliongoza mkutano huo.
Katika ardhi kubwa ya China wanaishi watu zaidi ya bilioni 1.4.
BEIJING - Wu Qian, msemaji wa ujumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China unaoendelea, siku ya Jumamosi alijibu maswali ya wanahabari na kujibu maswali kuhusu maoni na mapendekezo ya wajumbe wa majeshi hayo kuhusu jeshi, bajeti ya ulinzi ya China, na mauzo ya silaha ya Marekani kwa Taiwan ya China. Wakati wa majadiliano kwenye mkutano mkuu wa bunge la umma, wajumbe wa ujumbe wa kijeshi wamesema ni lazima kuimarisha ugavi wenye ufanisi kwa ajili ya uwezo wa hali ya juu wa kupigana vita, na kuufanya ulinzi wa taifa la China na vikosi vya jeshi kuwa vya kisasa kutokana na nguvu ya jumla ya nchi ya China, Wu amesema.
Kikao cha kufungwa kwa mkutano mkuu wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2024. (Xinhua/Ding Haitao) BEIJING – Mkutano mkuu wa pili wa mwaka wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambacho ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, kimefanya kikao chake cha kufungwa kwa mkutano huo leo Jumapili asubuhi ambapo Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamehudhuria kikao hicho kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.