Tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa mwaka wa Bunge la Umma la China yafanya mkutano wake wa tatu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 11, 2024

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la14 la China, akiongoza mkutano wa tatu wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2024. ( Xinhua/Xie Huanchi)

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la14 la China, akiongoza mkutano wa tatu wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING – Tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la Umma la 14 la China, imefanya mkutano wake wa tatu siku ya Jumapili ambapo Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo, aliongoza mkutano huo.

Mkutano huo umeamua kuwasilisha mswada wa marekebisho ya Sheria kuhusu muundo wa vyombo na utaratibu wa kazi wa Baraza la Serikali la China kwenye mkutano mkuu wa pili wa bunge hilo ili kupigiwa kura.

Mkutano huo umeamua kuwasilisha nyaraka tatu kwenye mkutano huo mkuu wa pili wa bunge kwa kujadiliwa na kuthibitishwa. Nyaraka hizo zinahusisha miswada ya maazimio kuhusu ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Mahakama ya Juu ya Umma ya China na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China.

Mkutano huo pia umejadili na kupitisha ripoti ya kushughulikia mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa bunge la umma la China kwenye mkutano huo mkuu wa bunge la umma.

Mwenyekiti mtendaji na Tume ya Wenyeviti walikutana kabla ya mkutano huo na kuandaa nyaraka.

Mkutano huo wa tume ya wenyeviti uliongozwa na Zhao, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China.

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya bunge hilo akiongoza mkutano wa pili wa wenyeviti watendaji wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya bunge hilo akiongoza mkutano wa pili wa wenyeviti watendaji wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha