Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakifanya mazungumzo huko Brasilia, Brazil asubuhi ya tarehe 20, Novemba. (Xinhua) China na Brazil zimeamua kuinua uhusiano wao kwenye jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa ajili ya dunia yenye haki zaidi na sayari endelevu zaidi.
(Picha inatoka tovuti ya CRI) Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden siku ya Jumamosi kando ya Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC) mjini Lima, Peru. Rais Xi amesema kuwa uhusiano kati ya China na Marekani umepitia kipindi cha misukosuko, lakini chini ya uongozi wa pamoja wa marais hao wawili, pande hizo mbili pia zimekuwa zikifanya mazungumzo na ushirikiano wenye ufanisi na kwa ujumla uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kwa utulivu.
RIO DE JANEIRO - Rais wa China Xi Jinping amewasili Rio De Janeiro, Brazil jana siku ya Jumapili kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa 19 wa Kilele wa G20 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Brazil kutokana na mwaliko wa Rais Luiz Inacio Lula da Silva. Rais Xi Jinping wa China akiwasili Rio de Janeiro kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa 19 wa G20 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Brazil kutokana na mwaliko wa Rais Luiz Inacio Lula da Silva, Novemba 17, 2024.
Rais wa China Xi Jinping akihudhuria hafla kubwa ya ukaribisho iliyoandaliwa na Rais wa Peru Dina Boluarte kwenye uwanja mbele ya Ikulu ya Lima, Peru, Mchana wa tarehe 14, Novemba kwa saa za Peru. (Xinhua/Xie Huanchi) Usiku wa Novemba 14 kwa saa za Peru, Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Peru Dina Boluarte walihudhuria hafla ya uzinduzi wa Bandari ya Chancay ya Peru kwa kupitia video.