Rais wa China Xi Jinping akikaribishwa kwa furaha na Waziri Mkuu wa Peru Gustavo Adrianzen na maofisa wengine waandamizi baada ya kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Callao huko Lima, Peru, Novemba 14, 2024. (Xinhua/Li Xueren) LIMA - Rais Xi Jinping wa China amesema Alhamisi kwamba anaamini kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, ziara yake hii itapeleka uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa China na Peru kwenye kiwango kipya, kuhimiza ushirikiano kati yao kupata matokeo halisi katika setka mbalimbali.
Rais Xi Jinping wa China siku ya Alhamisi alihudhuria hafla kubwa ya ukaribisho iliyoandaliwa na Rais Dina Boluarte wa Peru. Rais Xi aliwasili Peru mapema siku hiyo ili kufanya ziara ya kiserikali katika nchi hiyo na kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC).
Picha iliyopigwa Mei 16, 2024 ikionyesha barabara ya kuendesha gari kwa majaribio mjini ya Kampuni ya Teknolojia ya Volkswagen Tawi la China (VCTC) mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua) BEIJING - Asilimia zaidi ya 90 ya kampuni zinazowekezwa kwa mtaji wa kigeni nchini China zimeridhishwa na mazingira ya biashara ya nchi hiyo, kwa mujibu matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyotolewa jana Alhamisi.