Uchunguzi waonyesha asilimia zaidi ya 90 ya kampuni za kigeni zimeridhika na mazingira ya biashara ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2024

Picha iliyopigwa Mei 16, 2024 ikionyesha barabara ya kuendesha gari kwa majaribio mjini ya Kampuni ya Teknolojia ya Volkswagen Tawi la China (VCTC) mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)

Picha iliyopigwa Mei 16, 2024 ikionyesha barabara ya kuendesha gari kwa majaribio mjini ya Kampuni ya Teknolojia ya Volkswagen Tawi la China (VCTC) mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)

BEIJING - Asilimia zaidi ya 90 ya kampuni zinazowekezwa kwa mtaji wa kigeni nchini China zimeridhishwa na mazingira ya biashara ya nchi hiyo, kwa mujibu matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyotolewa jana Alhamisi.

Uchunguzi huo uliofanyika katika robo ya tatu ya mwaka huu miongoni mwa kampuni zaidi ya 400 za kigeni, pia umeonesha kuwa asilimia takriban 50 ya waliohojiwa wamesema wanaliona soko la China linavutia zaidi, kwa mujibu wa Sun Xiao, msemaji wa Baraza la Uhamasishaji Biashara ya Kimataifa la China.

Asilimia zaidi ya 60 ya kampuni za Marekani zilizofanyiwa uchunguzi zimesema mvuto wa soko la China kwa uwekezaji wa kigeni unaimarika zaidi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.26 kuliko robo iliyopita, amesema Sun.

Amesema kuwa asilimia karibu 20 ya kampuni hizo za kigeni zinapanga kuongeza uwekezaji nchini China, ikiwa ni ongezako la asilimia 2.07 kuliko robo iliyopita.

Asilimia takriban 54.76 ya kampuni hizo za kigeni zilizofanyiwa uchunguzi zinapenda kuongeza uwekezaji nchini China kwa kupanua mistari ya uzalishaji viwandani au kubadilisha muundo wake kuwa wa kidijitali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha