Feng Xingya, mwenyekiti wa kundi la kampuni za kuunda magari la China, GAC, amekuwa akifanya kazi katika tasnia ya magari kwa miaka zaidi ya 30. Ameshuhudia maendeleo ya tasnia ya magari ya China.
Katika mikutano mikuu miwili ya China inayoendelea mjini Beijing, yaani mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China na ule wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, toleo la Breli (maandishi ya watu wenye ulemavu wa macho) la ripoti ya kazi ya serikali ya nchi hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza kwa wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China. Wakati wa mchana wa jana Alhamisi, tarehe 5, Machi, mjumbe wa baraza hilo, Li Qingzhong kwenye kikao cha kikundi cha wajumbe wa sekta ya ustawi wa jamii na huduma za jamii, mahsusi aliomba kila mjumbe kuzingatia ripoti hiyo maalumu ya kazi ya serikali aliyokuwa ameishika mkononi wakati akizungumza.
ABA - Gexi Wangmu, ni mjumbe wa Bunge la 14 la Umma la China, anayefanya kazi kama mkurugenzi wa kituo cha matunzo ya wazee katika Mji wa Maerkang wa Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China. Akiwa ni mjumbe wa bunge hilo wa "kuzaliwa baada ya miaka ya 90", Gexi alianza maisha yake ya utumishi kama mfanyakazi wa mstari wa mbele wa huduma za matunzo ya wazee, na amejitolea kwa miaka 16 katika kazi yake hiyo.
NANJING - Sun Jingnan amekuwa akifanya kazi kama mchomeleaji vyuma katika Kampuni ya Vifaa vya Reli ya CRRC ya China Tawi la Nanjing kwa zaidi ya miongo mitatu, na pia shahidi wa maendeleo ya haraka ya sekta ya usafiri wa reli ya China. Akiwa amekua kutoka fundi kijana hadi kuwa mtaalamu, Sun ni mshauri na mlezi kitaaluma kwa vijana wengi wenye vipaji katika sekta hiyo ya reli.