Mjumbe wa Bunge la Umma la China adumisha mawasiliano na wakazi wazee kupitia huduma za matunzo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2025
Mjumbe wa Bunge la Umma la China adumisha mawasiliano na wakazi wazee kupitia huduma za matunzo
Gexi Wangmu (Kulia) akifahamishwa kuhusu huduma za afya za eneo husika alipomtembelea mwanakijiji mzee katika Kijiji cha Songgang cha Mji wa Maerkang, Eneo linalojiendesha la Makabila ya Watibet na Waqiang la Aba, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Februari 18, 2025. (Xinhua/Wang Xi)

ABA - Gexi Wangmu, ni mjumbe wa Bunge la 14 la Umma la China, anayefanya kazi kama mkurugenzi wa kituo cha matunzo ya wazee katika Mji wa Maerkang wa Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China.

Akiwa ni mjumbe wa bunge hilo wa "kuzaliwa baada ya miaka ya 90", Gexi alianza maisha yake ya utumishi kama mfanyakazi wa mstari wa mbele wa huduma za matunzo ya wazee, na amejitolea kwa miaka 16 katika kazi yake hiyo. Mwaka 2021, alitunukiwa tuzo ya "mfanyakazi bora wa matunzo ya wazee" na Idara ya Mambo ya Kiraia ya Mkoa huo wa Sichuan.

Kuanzia kuhakikisha huduma na chakula cha kila siku kwa wazee hadi kuwaongoza katika kufanya mazoezi ya kujenga mwili na kuwasaidia utunzaji wa kucha, Gexi amekuwa akiweka umuhimu sawa kwa vyote huduma za kihisia na kimwili kwa wazee wengi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha