人民网首页

Maandalizi

Mwandishi wa habari akipiga picha za eneo la mchanganyiko la Kijiji cha Olimpiki kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 huko Zhangjiakou, Mkoa wa Hebei Kaskazini mwa China, Januari 27, 2022. Vijiji vya Olimpiki kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 kile cha Yanqing, Mjini Beijing, Mji Mkuu wa China na kile cha Zhangjiakou mkoani Hebei, Kaskazini mwa China vimefungua rasmi milango yao kwa wanamichezo na maafisa wa timu kwa Michezo hiyo siku ya Alhamisi ya wiki hii. (Xinhua/Xiong Qi)

Vijiji vya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 vyafunguliwa rasmi

BEIJING - Vijiji vya Olimpiki kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 cha eneo la Yanqing, mjini Beijing na Zhangjiakou, Mkoa wa Hebei vilifungua milango yao kwa wanamichezo na maafisa wa timu kwa ajili ya Michezo hiyo siku ya Alhamisi ya wiki hii. Zhang Guannan, mfanyakazi wa timu ya uendeshaji wa Kijiji cha Olimpiki cha Beijing, amesema kijiji hicho kitawapokea wanamichezo 1,000 na maafisa wa timu kutoka nchi na kanda 44.

Wakati wa usiku wa Januari 27, washiriki na watu wa kujitolea wa maandalizi ya hafla ya kutunuku medali ya Michezo ya Olimpiki walifanya mazoezi ya mchakato wa utoaji medali.(Picha/Xinhua)

Washiriki Kwenye Maandalizi Wafanya Mazoezi ya hafla ya kutunuku medali ya Michezo ya Olimpiki

Kwa kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imekaribia, majaribio ya mwisho ya zana na vifaa na mazoezi ya mwisho ya mchakato mzima wa michezo hiyo yanafanyika kwenye uwanja wa utoaji wa medali wa Beijing, uwanja huo uko karibu na Uwanja wa Michezo wa Taifa “Kiota cha Ndege”.

Shughuli za Olimpiki haziathiriwa na hali ya janga la UVIKO-19

Mazoezi ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 yamefanyika kwenye Uwanja wa Taifa uitwao "Kiota cha Ndege," Januari 22, 2022. Takriban washiriki 4,000 walihusika katika mazoezi ya kila tukio la sherehe ya ufunguzi, wakijiandaa kwa sherehe ya ufunguzi itakayofanyika Februari 4.

Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi cha Zhangjiakou chakaribisha kundi la kwanza la ‘wakazi’

Kijiji cha Michezo ya Olimpiki cha Zhangjiakou ( Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing itafanyika hapa Beijing na huko Zhangjiakou, ndiyo maana kuna vijiji viwili vya michezo hiyo ) kilifunguliwa Januari 23 na kukaribisha kundi la kwanza la wakazi. Zaidi ya watu 40 wa ujumbe wa watangulizi wa michezo hiyo kutoka Australia, Uingereza, Kanada na nchi na kanda nyingine walifika na kukaa huko.

Iliyopita1 2