Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi cha Zhangjiakou chakaribisha kundi la kwanza la ‘wakazi’

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2022

Kijiji cha Michezo ya Olimpiki cha Zhangjiakou ( Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing itafanyika hapa Beijing na huko Zhangjiakou, ndiyo maana kuna vijiji viwili vya michezo hiyo ) kilifunguliwa Januari 23 na kukaribisha kundi la kwanza la wakazi. Zaidi ya watu 40 wa ujumbe wa watangulizi wa michezo hiyo kutoka Australia, Uingereza, Kanada na nchi na kanda nyingine walifika na kukaa huko.

Bendera za ujumbe unaoshiriki kwenye michezo hiyo zikipepea kwenye lango la Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi cha Zhangjiakou Desemba 22, Mwaka 2021. [Xinhua/Mpiga picha: Yang Fan]

Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi cha Zhangjiakou kiko eneo kuu la mashindano la Zhangjiakou, likichukua eneo la hekta 19.7, lililogawanywa kuwa eneo la makazi, eneo la uwanja na eneo la uendeshaji.

Katika Majengo yote ya Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi cha Zhangjiakou taa zake ziliwashwa kwa ajili ya kufanyiwa majaribio, Desemba 22, Mwaka 2021. [Xinhua/Mpiga picha: Yang Fan]

Siku hiyo, timu ya uendeshaji wa Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi cha Zhangjiakou ilifanya mchakato kamili wa kupokea wajumbe wa michezo ya olimpiki, kupima joto la mwili na kutumia dawa ya kuua virusi kwa mujibu wa utaratibu wa kazi na kanuni za udhibiti wa virusi vya korona, na kuongoza na kupanga kundi la kwanza la wakazi kuingia na kukaa kwa utaratibu.

Kwa upande wa vyakula na vinywaji, saa tano asubuhi ya siku hiyo, mgahawa wa wanamichezo ulianza kutoa huduma rasmi. Mapambo ya jadi ya China kama Taa Nyekundu na ukataji wa karatasi wenye kutengeneza picha za Michezo ya Olimpiki yalisifiwa na wajumbe wa kila ujumbe.  

Hali ya ndani ya mgahawa wa Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi cha Zhangjiakou Desemba 21, Mwaka 2021.[Xinhua/Mpiga picha: Yang Fan]

Kliniki iliyoko kwenye Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi cha Zhangjiakou nayo imefunguliwa vilevile. Kliniki hiyo ina jumla ya ghorofa nne. Baada ya kufunguliwa rasmi kwa kijiji hicho, kliniki hiyo inafanya kazi kwa masaa 24 kila siku na inaweza kutoa huduma kwa lugha mbalimbali kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kijerumani n.k.

Waandishi wa habari walifahamishwa kuwa Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi cha Zhangjiakou kitafunguliwa rasmi Januari 27 na kuendeshwa kwa siku 53 hadi Machi 16. Katika kipindi cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing, kijiji hiki kinatazamiwa kupokea wanamichezo na maofisa wa timu wapatao 2020 kutoka nchi na sehemu79. Wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing, kinakadiriwa kupokea wanamichezo na maofisa wa timu wapatao 644 kutoka nchi na sehemu 39. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha