BEIJING - Kituo cha Vyombo vya Habari cha mikutano mikuu miwili ya China ya Bunge la Umma la 14 la China na Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ambayo itaanza Machi 5 na 4, mtawalia, kimefunguliwa rasmi siku ya Jumanne. Kituo hicho kimesema, Waandishi wa habari zaidi ya 3,000 wamejiandikisha kuripoti mikutano hiyo mikuu miwili, wakiwemo zaidi ya 1,000 kutoka Hong Kong, Macao, Taiwan na nje ya nchi.