Kituo cha Vyombo vya Habari cha mikutano mikuu miwili ya China chafunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2024
Kituo cha Vyombo vya Habari cha mikutano mikuu miwili ya China chafunguliwa
Watu wakifanya kazi kwenye Kituo cha Vyombo vya Habari cha mikutano mikuu miwili ijayo ya China ya bunge la umma na baraza la mashauriano ya kisiasa mjini Beijing, China, Februari 27, 2024. (Xinhua/Li Xin)

BEIJING - Kituo cha Vyombo vya Habari cha mikutano mikuu miwili ya China ya Bunge la Umma la 14 la China na Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ambayo itaanza Machi 5 na 4, mtawalia, kimefunguliwa rasmi siku ya Jumanne.

Kituo hicho kimesema, Waandishi wa habari zaidi ya 3,000 wamejiandikisha kuripoti mikutano hiyo mikuu miwili, wakiwemo zaidi ya 1,000 kutoka Hong Kong, Macao, Taiwan na nje ya nchi.

Ukumbi wa mikutano na waandishi wa habari na vyumba vya mahojiano vya kituo hicho cha vyombo vya habari hapa vimetayarishwa kwa ajili ya mfululizo wa shughuli za mahojiano yatakayofanyika.

Kituo hicho pia kitatumia mtandao wa intaneti kutoa huduma na hatua mbalimbali ili kuleta hali ya kiurahisi zaidi kwa kazi ya waandishi wa habari wa ndani na nje ya China.

Matoleo ya kielektroniki ya nyaraka muhimu za mikutano hiyo yatatolewa kwa waandishi wa habari, na hivyo haina haja kwa waandishi wa habari kusubiri kuzichukua kwenye foleni ndefu eneo husika.

Vyumba vya mahojiano pia vitaandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wajumbe wa mikutano ya Bunge la Umma la China na Baraza la mashauriano ya kisiasa, vikitoa huduma zinazofaa kwa ajili ya mahojiano kati ya vyombo vya habari na wajumbe. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha