Liu Jieyi, msemaji wa mkutano wa pili wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) akishiriki kwenye mkutano na waandishi habari kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 3, 2024. (Xinhua/Li He) BEIJING – Mkutano wa mwaka wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambalo ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, unaanzia leo Jumatatu Machi 4 saa 9 alasiri (kwa saa za Beijing) hadi asubuhi ya Machi 10 mjini Beijing, msemaji wa mkutano huo Liu Jieyi alisema siku ya Jumapili kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) tarehe 29 Februari ilifanya mkutano kujadili rasimu ya “Ripoti ya Kazi ya Serikali” ambayo Baraza la Serikali la China litawasilisha kwenye Mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China ili ithibitishwe. Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping ameongeza mkutano huo.
Picha hii iliyopigwa Desemba 4, 2023 ikionyesha sehemu ya Barabara Kuu ya Wuxi-Zhenping katika Wilaya ya Wuxi, mjini Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Huang Wei) BEIJING - China imepata mafanikio makubwa katika kuboresha mtandao wake wa miundombinu ya usafiri na huduma za usafiri katika mwaka uliopita, Wizara ya Uchukuzi ya China imesema siku ya Jumatano ambapo thamani ya uwekezaji wa rasilimali zisizohamishika katika mfumo wa usafiri wa nchi hiyo ilifikia yuan trilioni 3.
BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 14 la China imehitimisha mkutano wake wa nane siku ya Jumanne mjini Beijing ambapo katika kikao cha kufunga, wajumbe wamepiga kura kupitisha Sheria iliyorekebishwa kuhusu kuhifadhi siri za nchi, na Rais Xi Jinping ametia saini amri ya rais ya kutangaza sheria hiyo. Zhao Leji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya bunge hilo la umma, aliongoza mkutano huo wa kufunga.