Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Ding Lin) BEIJING- Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye siku ya Ijumaa, ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo viongozi hao wawili wametangaza kuinua uhusiano wa pande mbili hadi kuwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Madagascar Andry Nirina Rajoelina ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Madagascar Andry Nirina Rajoelina siku ya Ijumaa, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir, ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Ding Lin) BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir siku ya Ijumaa, ambaye yuko hapa kuhudhuria Mkutano wa Kilele was 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na viongozi hao wawili kwa pamoja wametangaza kuinua hadhi ya uhusiano wa pande mbili hadi kuwa ushirikiano wa kimkakati.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa FOCAC. (Xinhua/Yan Yan) Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema China imekuwa mshirika wa kweli katika maendeleo ya Afrika, na ushirikiano kati ya Afrika na China utasaidia kujenga maendeleo na ustawi wa pamoja wa siku zijazo.