Marais wa China na Burundi watangaza kuinua hadhi ya uhusiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikutana an Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye yuko mjini Beijing kushiriki Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING- Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye siku ya Ijumaa, ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo viongozi hao wawili wametangaza kuinua uhusiano wa pande mbili hadi kuwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na Burundi umeshinda majaribu ya mabadiliko katika nyanja ya kimataifa na kwamba kuhimiza kila wakati uhusiano wa pande mbili ni kwa manufaa ya nchi zote mbili, na ni umuhimu wa kupigiwa mfano kwa nchi za Kusini kuwa na umoja na kujiimarisha zenyewe.

Rais Xi ameelezea matumaini yake kuwa nchi hizo mbili zitachukua utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa mwaka huu kama fursa ya kuimarisha uhusiano wao zaidi.

Amesema China iko tayari kuimarisha kuchangia uzoefu na ushirikiano katika ujenzi wa uwezo na Burundi katika maeneo kama vile mageuzi na maendeleo, ustawishaji wa vijijini na kutokomeza umaskini, na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja zikiwemo miundombinu, kilimo, uchumi na biashara.

Amesema China itaimarisha uratibu wa kimataifa na Burundi ili kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea na kuendeleza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

“Serikali ya Burundi imedhamiria kuendeleza maendeleo ya viwanda na kilimo cha kisasa ili watu waweze kuishi maisha bora” Rais Ndayishimiye amesema, akisisitiza mchango muhimu wa uungaji mkono wa China na ushirikiano na Burundi.

Amekaribisha kampuni zaidi za China kuwekeza nchini Burundi na kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika sekta ya madini, kilimo, miundombinu na nyanja nyinginezo.

Katika mkutano huo, pande hizo mbili zimetia saini nyaraka za ushirikiano wa pande mbili katika maeneo ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, ushirikiano wa kiuchumi, ushirikiano wa kilimo na mauzo ya kahawa nchini China. 

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye yuko mjini Beijing kushiriki Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha