Lugha Nyingine
Marais wa China na Sudan Kusini wainua hadhi ya uhusiano wa pande mbili
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir, ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Ding Lin)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir siku ya Ijumaa, ambaye yuko hapa kuhudhuria Mkutano wa Kilele was 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na viongozi hao wawili kwa pamoja wametangaza kuinua hadhi ya uhusiano wa pande mbili hadi kuwa ushirikiano wa kimkakati.
Rais Xi amesema, kujenga uhusiano thabiti na wenye nguvu kati ya China na Sudan Kusini kunaendana na matarajio ya pamoja na maslahi ya muda mrefu ya watu wa nchi hizo mbili.
Amesema China ina nia ya kuchangia uzoefu na fursa za maendeleo na Sudan Kusini, kuendelea kutekeleza miradi ya elimu, teknolojia na mingineyo, kuimarisha ushirikiano katika nyanja kama vile mafuta ya petroli, madini na kilimo, na kuisaidia Sudan Kusini kuwa na uchumi wa kutegemea sekta mbalimbali.
Rais Xi amebainisha kuwa, China inaiunga mkono Sudan Kusini katika kuendeleza kwa kasi mchakato wake wa mpito wa kisiasa na inapinga uingiliaji wa nje katika mambo yake ya ndani, akieleza matumaini yake kuwa Sudan Kusini itafikia mapema amani na maendeleo ya kudumu.
Rais Kiir amesema, shukrani kwa uungwaji mkono wa China, uchumi wa Sudan Kusini umeimarika na maisha ya watu yameboreka , huku akiongeza kuwa nchi yake itajitahidi kuweka mazingira salama na mazuri kwa kampuni za China.
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ambaye yuko mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 6, 2024. (Xinhua/Ding Lin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma