BEIJING - Viongozi waandamizi wa China Ijumaa walihudhuria vikao vya majadiliano katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, unaoendelea mjini Beijing, mji mkuu wa China. Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, Wang Huning ameshiriki katika kikao cha majadiliano cha kundi la wajumbe wa Bunge hilo kutoka Taiwan.
Kikao cha pili cha wajumbe wote cha Mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) kimefanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Ijumaa, Machi 7.
Katika mikutano mikuu miwili ya China inayoendelea mjini Beijing, yaani mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China na ule wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, toleo la Breli (maandishi ya watu wenye ulemavu wa macho) la ripoti ya kazi ya serikali ya nchi hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza kwa wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China. Wakati wa mchana wa jana Alhamisi, tarehe 5, Machi, mjumbe wa baraza hilo, Li Qingzhong kwenye kikao cha kikundi cha wajumbe wa sekta ya ustawi wa jamii na huduma za jamii, mahsusi aliomba kila mjumbe kuzingatia ripoti hiyo maalumu ya kazi ya serikali aliyokuwa ameishika mkononi wakati akizungumza.
Wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China jana Jumtano alasiri wamefanya vikao vya kujadili ripoti ya kazi ya serikali aliyotoa Waziri Mkuu wa China Li Qiang kwenye mkutano huo unaofanyika Beijing.