人民网首页

Picha

Mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) ukianza Machi 4, 2025 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.  Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine Li Qiang, Zhao Leji, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria kwenye mkutano huo. (Xinhua/Xie Huanchi)

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China laanza mkutano wake wa mwaka

BEIJING – Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambacho ni chombo kikuu cha mashauriano ya kisiasa cha China, imefanya mkutano wake wa mwaka Jumanne, Machi 4 mjini Beijing, China. Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine walihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa tatu cha Kamati hiyo ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC, uliofunguliwa saa 9 alasiri (kwa saa za Beijing) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Tume Tendaji na ajenda za mkutano vyaandaliwa tayari kwa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China

Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China Katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING – Wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China wamekusanyika mjini Beijing siku ya Jumanne kwenye kikao cha matayarisho cha mkutano wa tatu wa bunge hilo la 14 la China utakaoanza leo Jumatano, ili kuchagua Tume Tendaji wa mkutano na kupanga ajenda zake.

Kujua demokrasia ya umma ya China ya mchakato kamili

Demokrasia ni thamani ya pamoja ya binadamu wote, na ni wazo muhimu linaloshikiliwa siku zote na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na watu wa China. Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha CPC ulipofanyika mwaka 2012, kamati kuu ya Chama ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiini chake imefahamisha kwa kina kuhusu kanuni ya maendeleo ya siasa ya kidemokrasia ya China, ikitoa wazo la demokrasia ya umma ya China ya mchakato kamili na kulihimiza kwa nguvu.

Mkutano wa Kamati ya Wajumbe wa Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wafungwa

Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akiongoza na kutoa hotuba kwenye mkutano wa 10 wa Kamati ya wajumbe wa kudumu ya Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC uliofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 2. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING - Kamati ya 14 ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambayo ni chombo cha kitaifa cha China cha mashauriao ya kisiasa, imemaliza mkutano wa kumi wa kamati yake ya wajumbe wa kudumu mjini Beijing jana Jumapili.

Iliyopita1 2 3 4 Inayofuata