ABA - Gexi Wangmu, ni mjumbe wa Bunge la 14 la Umma la China, anayefanya kazi kama mkurugenzi wa kituo cha matunzo ya wazee katika Mji wa Maerkang wa Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China. Akiwa ni mjumbe wa bunge hilo wa "kuzaliwa baada ya miaka ya 90", Gexi alianza maisha yake ya utumishi kama mfanyakazi wa mstari wa mbele wa huduma za matunzo ya wazee, na amejitolea kwa miaka 16 katika kazi yake hiyo.
NANJING - Sun Jingnan amekuwa akifanya kazi kama mchomeleaji vyuma katika Kampuni ya Vifaa vya Reli ya CRRC ya China Tawi la Nanjing kwa zaidi ya miongo mitatu, na pia shahidi wa maendeleo ya haraka ya sekta ya usafiri wa reli ya China. Akiwa amekua kutoka fundi kijana hadi kuwa mtaalamu, Sun ni mshauri na mlezi kitaaluma kwa vijana wengi wenye vipaji katika sekta hiyo ya reli.
Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akiongoza mkutano wa 38 wa Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la 14 la Umma la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Februari 17, 2025. (Xinhua/Yao Dawei) BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Bunge la 14 la Umma la China itafanya mkutano wake wa 14 mjini Beijing Februari 24 na 25.