BEIJING —Septemba 2, Semina juu ya Stadi za Eneo la Afrika Kuhudumia Mikakati ya Kitaifa na Ujengaji wa Uwezo wa Mawasiliano ya Kimataifa wa Taasisi ya Washauri Bingwa wa China-Afrika ilifanyika Beijing. Miongoni mwa washiriki alikuwa Liu Hongwu, Mkuu wa Taasisi ya Stadi za Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, ambaye ametumia miongo minne akifanya stadi mbalimbali kuhusu Afrika.
Balozi wa Burundi nchini China, ambaye pia ni mwakilishi wa nchi inayoshikilia uenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, Télesphore Irambona, ametangaza kwamba Ubalozi wa Burundi mjini Beijing utafanya Wiki ya Utamaduni wa Burundi ambayo ni ya kwanza kabisa kufanyika, ikihusisha shughuli mbalimbali. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Burundi Juni 12, Balozi Irambona alieleza kuwa mfululizo wa shughuli za Wiki hiyo ya Utamaduni wa Burundi zenye kaulimbiu isemayo "Ngoma Takatifu ya Burundi (Ingoma) Inapoimarisha Uhusiano wa Kiutamaduni kati ya China na Afrika" zitafanyika jijini Beijing kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 1 Julai, zikihusisha kwa sehemu kubwa maonyesho ya kiutamaduni, kongamano la uwekezaji, na maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa Burundi.
Chuma Mohamed Muhibu, mwanafunzi Mtanzania mwenye umri wa miaka 35, kwa sasa anasoma shahada ya uzamivu (PhD) katika Sera na Vitendo vya Elimu ya Walimu (Teacher Education Policy and Practice) katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing nchini China. Imepita miaka saba tangu alipofika China kwa mara ya kwanza mwaka 2019 kwa ajili ya masomo yake.
Mjumbe wa Baraza la Mamlaka ya Mpito la Sudan, Abdullah Yahya amesema, Sudan na China zinafurahia uhusiano uliokita mizizi ya kina uliojengwa katika uhusiano wa kimkakati na wa kunufaishana. Akizungumza katika tukio la “Asante, China” lililofanyika Port Sudan, mashariki mwa Sudan juzi Jumatatu, Yahya ameeleza mchango muhimu wa China katika miradi ya miundombinu nchini Sudan, hususan katika maendeleo ya barabara, madaraja, mabwawa na vituo vya kuzalisha umeme.