Lugha Nyingine
Sudan na China zinafurahia uhusiano wa kimkakati wenye mizizi ya kina: Afisa wa Sudan
Mjumbe wa Baraza la Mamlaka ya Mpito la Sudan, Abdullah Yahya amesema, Sudan na China zinafurahia uhusiano uliokita mizizi ya kina uliojengwa katika uhusiano wa kimkakati na wa kunufaishana.
Akizungumza katika tukio la “Asante, China” lililofanyika Port Sudan, mashariki mwa Sudan juzi Jumatatu, Yahya ameeleza mchango muhimu wa China katika miradi ya miundombinu nchini Sudan, hususan katika maendeleo ya barabara, madaraja, mabwawa na vituo vya kuzalisha umeme.
Pia ametoa wito kwa kampuni za China na taasisi za kifedha kupanua uwekezaji na uhusiano na wenzao wa Sudan, akiahidi uungaji mkono kamili kutoka upande wa Sudan.
Kaimu Balozi wa China nchini Sudan Xu Jian alihudhuria tukio hilo, akilielezea kuwa ni sehemu muhimu ya Mwaka wa Mabadilishano ya kati ya Watu na Watu wa China na Afrika, na kueleza matumaini yake kwa urafiki imara zaidi wa pande mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



