Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akiongoza kikao cha kufungwa cha mkutano wa 15 wa Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya CPPCC na kutoa hotuba kwenye kikao hicho mjini Beijing, China, Machi 2, 2026. (Xinhua/Ding Lin) BEIJING - Mkutano wa 15 wa Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambalo ni chombo kikuu cha ushauri wa kisiasa cha China, umefungwa jana Jumatatu mjini Beijing.
Zhang Fan ni naibu meneja mkuu wa Kundi la Zana na Vifaa vya Umeme la China ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Zhang anaona kuwa "teknolojia ya AI pamoja na viwanda vya utengenezaji bidhaa" vitaweza kutimizwa kwa kupitia kufanya mpango wa jumla kuhusu utendaji wa pande mbalimbali na kwenye ngazi tofauti.
Dong Hongtao ni fundi wa treni za mwendo-kasi wa Kampuni ya Kundi la Reli la Xi'an la China, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Tangu ajiunge na kazi ya matengenezo ya treni za mwendo-kasi (EMU) mwaka 2007, Dong amekuwa akiongoza timu yake kufanyia matengenezo seti zaidi ya 120,000 za treni hizo na kushughulikia hitilafu zaidi ya 3,000.
Kituo cha Habari cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) na Mkutano wa Nne wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambayo inafahamika kwa jina la “Mikutano Mikuu Miwili ya Mwaka ya China” kimefunguliwa rasmi leo Ijumaa mjini Beijing, na kinatarajiwa kutoa huduma kwa waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi watakaofuatilia. Mikutano hiyo inatarajiwa kuanza mjini Beijing Machi 5 na Machi 4, mtawaliwa.