Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China umefunguliwa rasmi leo Machi 4 saa tisa mchana katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Katika mkutano wa siku saba, wajumbe 2,078 kutoka nyanja 34 ikiwemo uchumi, utamaduni, elimu na raslimali za mazingira watasikiliza na kupitia ripoti ya kazi ya baraza hilo na ripoti kuhusu kazi ya utoaji mapendekezo, huku wakihudhuria mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la Taifa, kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali na ripoti nyingine husika, kujadili mswada wa mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii.
Jin Ruirui, mkuu wa shirikisho la mafundi wa kudarizi la kabila la Wayi la ngazi ya kiwilaya katika Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, amekuwa akijikita katika kuhifadhi ufundi huo wenye historia ya miaka zaidi ya elfu moja, wakati huohuo amewaongoza mafundi wenyeji wa kudarizi kuelekea ustawi wa kitamaduni na ustawishaji wa vijiji. Ufundi huo wa kudarizi wa kabila la Wayi wenye historia ya miaka ya zaidi 1,300, unajulikana kwa udarizi wake wa michoro na picha za kupendeza na mbinu mbalimbali za kudarizi, na umekuwa kibebaji muhimu cha utamaduni wa kabila la Wayi.
Liu Jieyi, msemaji wa mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 3, 2026. (Xinhua/Wang Xi) BEIJING - Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambacho ni chombo cha juu cha ushauri wa kisiasa cha China, itafanya mkutano wake wa nne wa mwaka Tarehe 4 hadi Tarehe 11 mwezi huu mjini Beijing, msemaji wa mkutano huo Liu Jieyi amesema.
Guo Hongjing anafanya kazi ya mkuu wa timu ya vipuri vya vifaa katika idara ya ghala ya Kampuni ya Matairi ya Tianjin Lizhong mjini Tianjin, kaskazini mwa China. Kazi yake ya kila siku ni kupokea, kutoa na kukagua raslimali ndani ya ghala.