

Lugha Nyingine
Korosho za Ruvuma, Mtwara na Lindi kusafiriswa kupitia bandari ya Mtwara
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameagiza kuwa korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara kwa kuwa serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia amewaagiza viongozi wa bandari wapitie tozo zote zinazowakwaza wasafirishaji ili kuwavutia kuitumia bandari hiyo .
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa wakulima wakubali kupokea pembejeo kulingana na mahitaji yao na watalipia kulingana na idadi ya mifuko waliyochukua na sio shilingi 110 kwa kila kilo kama inavyelezwa
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wadau wote wa korosho nchini katika kufanikisha mkakati huo ikiwemo kutengeneza mashine za ubanguaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma