Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2021

Tovuti ya Gazeti la Umma ilizinduliwa tarehe 1 Januari 1997, na ni jukwaa kubwa la utoaji wa habari la gazeti la umma la China. Pia ni kampuni ya habari na utamaduni iliyo chini ya usimamizi wa gazeti la Umma.

Tarehe 27 Aprili 2012, Tovuti ya Gazeti la Umma iliorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Shanghai, na kuwa tovuti ya kwanza ya chombo cha habari cha China kuorodheshwa kwenye soko la Hisa la China.

Licha ya toleo la kichina, Tovuti ya Gazeti la Umma ikiwa ni moja ya vyanzo habari kwenye mtandao wa Internet pia inatoa matoleo ya lugha 7 za makabila madogo na lugha 9 za nchi za nje zikiwemo Kiingereza, Kirusi, kifaransa, kihispania na Kiarabu. Mpaka sasa, ina matawi 33 katika China bara na ofisi 15 katika miji mbalimbali duniani ikiwemo Hong Kong, Tokyo, New York, San Francisco, Seoul, London, Moscow, Johannesburg, Sydney, Paris, Stockholm na Bangkok.

Viongozi wa China wanatilia maanani sana maendeleo ya Tovuti ya Gazeti la Umma. Tarehe 25 Januari 2019, ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China imefanya kikao kuhusu maendeleo ya muungano wa vyombo vya habari na zama za vyombo vyote vya habari, ambapo rais Xi Jinping wa China aliendesha kikao hicho na kutoa hotuba akisisitiza juhudi za kustawisha vyombo vya habari na kupaza sauti kuu katika mawasiliano ya umma.

Tarehe 19 Februari 2016, rais Xi Jinping alifanya ziara kwenye ofisi za Gazeti la Umma. Katika studio ya Tovuti ya Gazeti la Umma, rais Xi alifanya mazungumzo kwa njia ya video na wanakijiji wa Chixi, mji wa Ningde, mkoani Fujian, kusini mashariki mwa China.

Tarehe 20 Juni 2008, aliyekuwa rais wa China Hu Jintao alifanya ziara kwenye ofisi za Gazeti la Umma na kufanya mawasiliano na watu kupitia ukurasa wa baraza la Qiangguo katika Tovuti ya Gazeti la Umma.

Tarehe 26 Aprili 2000, aliyekuwa rais wa China Jiang Zemin alitembelea Tovuti ya Gazeti la Umma kufuatilia habari kuhusu ziara yake nchini Afrika Kusini.

Tarehe 1 Julai mwaka 2006, tovuti ya www.cpcnews.cn inayoendeshwa na Tovuti ya Gazeti la Umma ilizinduliwa, na kuwa tovuti rasmi ya kueneza na kufahamisha mawazo, nadharia, sera na habari kuhusu chama cha kikomunisti cha China.

Kwa kuzingatia maudhui ikiwa ni kazi yake ya msingi, na kulenga shughuli za akili, Tovuti ya Gazeti la Umma inajitahidi kuwa kampuni inayoongoza katika ConTech kwa kuendeshwa na mtaji na teknolojia, ili kuongeza ushawishi na nguvu yake ya ushindani.

Katika upande wa maudhui, Tovuti ya Gazeti la Umma imelenga shughuli kwenye pande nne. Kwanza, kuzingatia maudhui halisi, kutilia maanani tahariri, maoni, hadithi za kina, uchambuzi na mapendekezo ya utungaji wa sera, ili kuimarisha nguvu ya ushindani ya maudhui yake na kuwa na ushawishi kwenye maoni ya umma.

Pili, kujenga jukwaa linalosaidia idara za serikali, makampuni na taasisi za umma, vyuo vikuu na taasisi za utafiti kukabiliana na changamoto katika zama ya vyombo vyote vya habari.

Tatu, kutoa huduma za udhibiti wa hatari kwa makampuni ya mtandao wa Internet kwa kutumia teknolojia ya akili bandia, na kuanzisha ajira mpya, sekta mpya, kigezo kipya na jukwaa jipya kupitia jukwaa la kudhibiti hatari na utoaji wa mafunzo.

Mwisho, ni kujenga mtandao wa kukusanya na kusambaza maudhui, na kuwa jukwaa la kati la kuwaunganisha watoa maudhui na watumiaji wa maudhui, na kutoa huduma za kubadilishana na kiufundi kwa pande zitakazohusika.

Mtandao wa Gazeti la Umma unatoa kipaumbele kutoa huduma kwenye simu za mkononi. Bodi ya kutoa ujumbe kwa viongozi iliyoanzishwa mwaka 2006 imesaidia kutatua maombi zaidi milioni 1.5 ya watumiaji wa mtandao wa Internet, na kuwa mfano mzuri wa upana, ukweli na ufanisi wa demokrasia ya kisoshiolisti yenye umaalumu wa China. App ya “Ujenzi wa Chama” imekuwa jukwaa la kuwahudumia wanachama wa chama cha kikomunisti cha China na idara za chama katika ngazi mbalimbali kutangaza mambo ya ujenzi wa chama, kutoa mafunzo, kusimamia shughuli za chama na kufanya mawasiliano. Vilevile, app ya video fupi “People’s Video” inalenga kujenga jumuiya ya video yenye akili kwenye msingi wa 5G.

Baada ya maendeleo ya miaka mingi, Tovuti ya Gazeti la Umma imejenga mfumo wa ConTech ikiwemo viwango vitatu vya utafiti wa msingi, uungaji mkono wa kiufundi, na matumizi ya kimazingira.

Ikiwa imeidhinishwa na wizara ya sayansi na teknolojia, maabara ya utambuzi wa mambo ya uenezi inayojengwa na Tovuti ya Gazeti la Umma imetoa matokeo imara ya utafiti wa kimsingi kwa ajili ya kutimiza kupata maendeleo makubwa katika teknolojia muhimu ya muunganiko wa vyombo vya habari.

Majukwaa kama vile injini ya akili bandia, jukwaa la uwezo wa video, jukwaa la kukusanya na kueneza yametoa uungaji mkono wa kiufundi kwa Tovuti ya Gazeti la Umma.

Aidha, Tovuti ya Gazeti la Umma imetumia shughuli zake mbalimbali za uvumbuzi, uendeshaji, udhibiti wa hatari na kukusanya na kueneza habari, kutimiza mageuzi ya uwezo kiviwanda.

Tovuti ya Gazeti la Umma ina matawi kadhaa ikiwemo Peopleyun.cn, Huanqiu.com, Haiwainet.cn, People’s Capital, People's Sports, People's Technology, People's Health, na People's Video.

Mfuko ulio chini ya tovuti hiyo umewekeza kwenye miradi kadhaa, na mradi wa kwanza katika nchi za nje uliingia kwenye soko la hisa la Nasdaq mwezi Septemba mwaka 2018.

Tovuti ya Gazeti la Umma imejenga kundi lenye watu wenye sifa bora na utamaduni wa kampuni. Imepata tuzo ya habari ya China mara 14 na kuorodheshwa kwenye vyombo vya habari 500 duniani kwa miaka mingi kutokana na hali yake ya uaminifu, ushawishi na nguvu ya kusambaza habari.

Tovuti ya Gazeti la Umma italenga kuwa kampuni inayoongozwa kwenye Contech, kufanya juhudi zote katika thamani yake ya kisiasa, thamani ya uenezi, thamani ya chapa, thamani ya jukwaa na thamani ya mitaji, kujibadilisha kuwa kampuni yenye teknolojia na akili, kujitahidi kuwa uenezi wenye taaluma zaidi ya sauti za China na mlinzi thabiti wa maslahi ya watu wa China.

Tovuti ya Gazeti la Umma inaendesha akaunti za lugha mbalimbali katika vyombo vya habari vya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter, YouTube, VK na Line. Idadi ya watu wanaofuatilia ukurasa wa facebook na Twitter wa Gazeti la Umma imezidi milioni 100.

Tovuti ya Gazeti la Umma inashirikiana na vyombo vya habari vya nchi za nje kwa mapana. Ushirikiano kati yao ni pamoja na ubadilishanaji wa habari, ushirikiano wa akiba ya data, ujenzi wa pamoja wa chaneli na vipindi, utengenezaji na uenezi wa pamoja wa vipindi vya televisheni. Kampuni zake katika nchi za nje zimefanya shughuli mbalimbali za kiuchumi, kiufundi na kitamaduni ili kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya China na nchi za nje.

(Kusasishwa Machi 2020)

Toleo la Kiswahili la Tovuti ya Gazeti la Umma

Anwani: New Media Tower of People's Daily, No.2 Jintai Xilu, Chaoyang District, Beijing, China

Fax: +8610-65363688 

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha