Tanzania: Mazingira ya uwekezaji na biashara ni salama

(CRI Online) Mei 25, 2021

Serikali imesema mwamko wa biashara na uwekezaji ni mkubwa kwa sasa baada ya baadhi ya makampuni na taasisi zilizokuwa zimefunga shughuli zao kuanza kurejea, na kwamba serikali kwa sasa inapitia upya sera yake ya uwekezaji ili kuweka mazingira bora zaidi ya biashara na uwekezaji.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jana jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania,Jeroen Verheul, na kuongeza kuwa tamko la rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuhusu kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara yanakuwa Rafiki.

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania amekiri kuwa Tanzania ina fursa na rasilimali nyingi zinazohamasisha na kuvutia biashara na uwekezaji licha ya uwepo wa maeneo machache yanayohitaji maboresho . Kulingana na balozi, endapo maeneo haya yataboreshwa, makampuni mengi kutoka ulaya yatakuja kuwekeza.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha