

Lugha Nyingine
SOKA: OLE Gunnar asema anahitaji kuongeza nyota wapya watatu ndani ya kikosi chake
Kocha Mkuu wa Manchester United OLE Gunnar Solskjaer, amesema anahitaji kuongeza nyota wapya watatu ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao. Kocha huyo ambaye msimu huu alikuwa katika ubora wake hasa mechi za ugenini ambapo hawajafungwa mchezo wowote kati ya 19 anahitaji kuongeza nguvu zaidi ili aweze kushindana na mpinzani wake mkubwa Manchester City. Katika Ligi Kuu England, United imekamilisha msimu kwa kujikusanyia jumla ya pointi 74 ikiwa ni namba mbili huku City ikiwa ni namba moja na pointi zao ni 86. Mchezo wao wa mwisho kwa msimu United ilishinda jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Wolves. Kocha huyo amesema kwa sasa wanaangalia kwenye kikosi chao wachezaji gani watasalia na ambao wanatakiwa kuondoka na pia wale watakaotoka kwenda kupata uzoefu. Amesisitiza kwamba matumaini yake ni kuboresha kikosi, na kwamba anahitaji wachezaji wawili ama watatu ndani ya kikosi chake.
Aina nane maarufu zaidi za maua ya Yunnan hakika kuna moja inayokushangaza zaidi
Korongo wacheza kwenye uwangja wa juu hali ya viumbe yaendelea vizuri mkoani Tibet
Rasilimali ya utamaduni yasukuma mbele ujenzi wa kijiji cha kupendeza cha Luquan mjini Shijiazhuang
Mji wa Zhengzhou warudia katika hali ya kawaida ya uzalishaji na maisha
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma