China yatangaza kumuwekea vikwazo Jonnie Moore

(CRI Online) Mei 27, 2021

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian ametangaza kuwa China imeamua kumzuia mjumbe wa Kamati ya uhuru wa kidini ya kimataifa ya Marekani Johnnie Moore na jamaa zake kuingia China bara, Hongkong na Macau.

Bw. Zhao amesema hayo alipokuwa akizungumzia ripoti ya kimataifa ya mwaka 2020 juu ya kuamini dini inayohusu hatua ya kumuwekea vikwazo ofisa mmoja wa China ambayo ilitangazwa hivi karibuni na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Bw. Zhao pia amesema China inaihimiza Marekani isahihishe makosa yake, kuondoa vikwazo na kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya China kwa kutumia suala la dini.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha