Watafiti wa Marekani wagundua mfumo wa kukinga kuzeeka kwa panya

(CRI Online) Mei 27, 2021

Watafiti wa Marekani wagundua mfumo wa kukinga kuzeeka kwa panya

(GMT+08:00) 2018-08-01 09:36:51

Watafiti wa Marekani wameripoti kuwa kurejesha uwezo wa jeni za mitochondria zinazoharibuka kunaweza kuponesha panya wanaojitokeza na kunyanzi na kupoteza nywele. Matokeo ya utafiti huo yanatarajiwa kutoa wazo jipya kwa tiba ya kinga ya uzeekaji.

Mitochondria inaweza kuzalisha nishati kwa seli, ambayo inaitwa kiwango cha kuzalisha umeme cha seli. Utafiti umeonesha kuwa tatizo la uwezo wa mitochondria linahusiana na uzeekaji.

Utafiti huo uliotolewa kwenye jarida la Uingereza "Kifo na Maradhi ya Seli" umesema, watafiti hao wametumia Doxycycline kuharibu DNA ya mitochondria. Antibiotic ya aina hiyo inaweza kufanya kimeng'enya kinachotengeneza DNA kupoteza uhai. Baada ya wiki nne hadi nane, panya hao wanajitokeza na dalili za kunyanzi na kupoteza nyweli.

Watafiti wamesema, dalili hizo zinafanana na uzeekaji wa binadamu unaotokana na uvutaji sigara. Baada ya kusimama kutia doxycycline kwenye chakula chake, panya hao wameanza kupona. Jaribio hilo limethibitisha kuwa kupoteza nywele na uzeekaji wa ngozi unaweza kupona.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha