Anne akiwa mkoani Xinjiang: Kuangalia utamaduni wa ajabu wa Kijiji cha Lop Nur

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2021

 

(picha zinatoka:Tovuti ya Gazeti la Umma)

Kijiji cha Umma cha Lop Nur kiko katika Wilaya ya Yuli, mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur ulioko kaskazini magharibi mwa China, ambapo Mto Tarim unapitia jangwani na msitu wa mipoplar unaonekana juu ya mawimbi yanayong’ara.

Watu wa Lop Nur, ni moja ya makundi ya zamani kabisa ya watu walioishi katika jangwa la Taklamakan, wakitegemea uvuvi kwa kujikimu na kujenga utamaduni wa kipekee kutokana na mtindo wao wa maisha. Mji wa Yuli ni maarufu kutokana na mandhari yake ya asili na utamaduni wa kabila, na unaendelea kuvutia watalii wengi kutoka nchini na ng’ambo.

Hivi sasa watu wengi zaidi wa Lop Nur wameacha baadhi ya desturi zao za jadi. Lakini bado kuna wenyeji wachache wanaoendelea kufuata mila na desturi zao za uvuvi na kutumia miti ya mipoplar kutengeneza ngalawa. Jiunge na Anne, wakati tukiangalia utamaduni wa ajabu katika kijji cha Lop Nur.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha