Kenyatta asifu Ethiopia kwa kukaribisha Safaricom

(CRI Online) Juni 11, 2021

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Jumanne ameisihi Ethiopia kufungua sekta yake ya mawasiliano kwa wawekezaji wa makampuni binafsi ya kubadilishana pesa kwa njia ya simu, hatua ambayo huenda ikaimarisha hatua zilizopigwa kwenye sekta hiyo na kuvutia uwekezaji wa kigeni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Kenyatta ameyasema hayo mjiji Addis Ababa wakati akiwa ziarani nchini humo. Jopo la makampuni kadhaa yakiongozwa na Safaricom ya Kenya yalipewa leseni ya kuanza biashara ya ubadilishanaji fedha kwa njia ya simu nchini Ethiopia ambapo sasa hivi ni kampuni ya Ethio Telecom pekee, inayotoa huduma hiyo.

Kenyatta amesifu hatua hiyo akisema kuwa itatoa nafasi mpya za ajira kwa mamilioni ya watu wa Ethiopia. Huduma ya pesa kwa njia ya simu ilianzishwa nchini Kenya takriban muongo mmoja uliyopita lakini sasa inatumika kwenye mataifa mengi yalioko chini ya jangwa la Sahara.

Safaricom imepanga kuwekeza hadi dola bilioni 8.5 kwenye sekta ya mawasiliano nchini Ethiopia miongoni mwa mambo mengine. Ethiopia pia inapanga kuuza asilimia 40 ya hisa za Ethio Telecom kwa wawekezaji wa kibinafsi pamoja na nyingine asilimia 5 kwa wananchi wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha