Wizara ya Fedha Uganda yatangaza hatua mpya za sera za ushuru

(CRI Online) Juni 11, 2021

Ili kuongeza ukusanyaji wa mapato na kulinda serikali kutokana na kikwazo cha kuongezeka kwa deni la umma, Wizara ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi nchini Uganda imetangaza hatua mpya za sera za ushuru.

Akiwasilisha Bajeti ya Kitaifa ya mwaka wa Fedha 2021/22,jana, waziri mteule wa nchi wa Mipango, ,Bwana Amos Lugoloobi katika uwanja wa Kololo alisema mapato ya ndani kwa mwaka ujao wa fedha yanakadiriwa kuwa Sh22.425 trilioni, sawa na asilimia 13.8 ya Pato la Taifa, ikilinganishwa na malipo yaliyotajwa ya Sh19.432 trilioni, sawa na asilimia 13.1 ya Pato la Taifa katika mwaka wa fedha 2020/21.

Ili kufanikisha mapato yaliyotajwa katika bajeti ya kitaifa ya 2021/22, Bwana Lugoloobi alisema hatua za sera zitakazotekelezwa katika mwaka huo wa fedha ni pamoja na ushuru wa mageuzi ya mapato ya nyumba za kukodisha,kunguza viwango vya kushuka kwa thamani kwa baadhi ya mali, kusitisha upunguzaji wa wakati mmoja wa posho za awali na uchakavu katika mwaka wa kwanza wa matumizi ya mali zinazostahili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha